FAHAMU MAANA NA UMUHIMU WA ISIMU YA LUGHA (LINGUISTICS)

Je, umewahi kujiuliza ni  ala (instruments) zipi zinahusika kutamka sauti  fulani?  Sauti  ni  kitamkwa ambacho huoneshwa kwa alama ya umbo fulani, mfano /b/, /p/,/m/ n.k. Nini basi kinafanyika kuvitofautisha vitamkwa au sauti mbili zinazotamkiwa sehemu moja, kwa mfano /b/ na /p/? Je, umewahi kujiuliza kwa nini watu wengine, kama bubu, hawawezi kuongea? Kwanini neno moja katika lugha fulani lina maana nyingi na halileti utata? Kwanini watu wengine hawezi kuitamka sauti fulani? Kwa mfano, Wahaya huwawia vigumu kutamka sauti ng' /ŋ/ katika maneno kama vile ng'ombe,ng'ang'ana; Wakurya  /l/ katika  neno  kula; Wasukuma /r/ katika neno kura, kwa kutaja baadhi. Je, uhusiano wa lugha na jamii ni upi? Maswali hayo na mengine mengi ndio huwafanya wanaisimu (linguists) kushughulika kila kuchapo kwa kufanya tafiti mbalimbali ili kutafuta majibu ya maswali hayo. Soma zaidi...

One Comment on FAHAMU MAANA NA UMUHIMU WA ISIMU YA LUGHA (LINGUISTICS)

  • Alcheraus Mushumbwa -

    Nimependa na kufurahia, na kupata maarifa kutoka katika makala yenye mada ya 'FAHAMU MAANA NA UMUHIMU WA ISIMU YA LUGHA (LINGUISTICS). ' Ni jambo la kheri kutufunza na kutujuza kupitia tovuti hii. Ushauri wangu ni kuwa angalia uwezekano wa kufungua JARIDA LA ISIMU NA LUGHA ambalo linakuwa linachapisha makala mbalimbali zihusuzo Isimu, Fasihi, Lugha na Utamaduni. Mnaweza kuwa mnatoa matangazo ya kualika wasomi, wataalam na wadau wa lugha, sanaa na utamaduni kuwa wanaandika makala na kuzituma kwenu kisha kupitia kamati maalumu ya uhariri wa makala inazipitia na zile zinazoonekana kuwa bora kulingana na vigezo mnavyokuwa mmeweka zinachapishwa; na jarida, linatoka kila mwaka au nusu mwaka na kuuzwa kwa wapenda lugha. Hii ni njia mojawap ya Idara kujiongezea kipato sanjari na kusambaza maarifa kwa watu wengi tena wa maeneo mbalimbali, lakini pia, inatangaza na kukipa umaarufu chuo cha CARUMCO.Vyuo, kama UDSM kupitia TATAKI wanayo hadi hivi sasa majarida matatu ( Mulika, Kioo cha Lugha na Kiswahili) ambayo hutoka kila mwaka na makala zinazochapishwa mule huwa ni za wadau mbalimbali wa lugha na utamaduni kutokana na mwaliko unavyowataka wafanye hivyo. Pia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wanayo majarida kadhaa ambayo wadau huchangia mawazo yao kupitia makala, na moja wapo ya mada zinazochapishwa mule ni zinahusu lugha, fasihi na sanaa.

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *